Polisi ajeruhiwa katika makabiliano na washukiwa wa ugaidi Lamu

Polisi ajeruhiwa katika makabiliano na washukiwa wa ugaidi Lamu

by -
0 533

Lamu,KENYA:Afisa mmoja wa polisi katika eneo la Mangai kaunti ya Lamu amejeruhiwa vibaya wakati wa makabiliano baina ya polisi na washukiwa wa kundi la kigaidi la al-shabaab.

Inasemekana jumatano asubuhi washukiwa hao walijaribu kuvamia kambi ya polisi wa kushughulikia visa vya dharura RDU iliyoko eneo la Mangai-Lamu Mashariki .

Msemaji wa jeshi la Kenya-KDF kanali David Obonyo ameambia Baraka Fm kuwa washukiwa hao wametorokea msitu wa Boni baada ya kuzidiwa nguvu na maafisa wa usalama.

Obonyo ameongeza kuwa maafisa wa Kdf wanashirikiana na walinda usalama wengine kuwasaka waliotekeleza uvamizi huo.

Kwa sasa polisi inasema hali ya usalama imeimarishwa huku ikishauri wakaazi wa eneo hilo kuripoti mtu wanayemshuku kuwa tishio kwa usalama.

Imehaririwa na Joseph Jira

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES