Idara ya polisi yafanya mabadiliko

Idara ya polisi yafanya mabadiliko

by -
0 318

NAIROBI,KENYA:Idara ya polisi imetangaza mabadiliko miongoni mwa maafisa 64 wakuu wa polisi kote nchini.

Katika mabadiliko hayo yaliyofanywa na naibu inspekta mkuu wa polisi Joel Kitili, ukanda Pwani na Garisa ni miongoni mwa maeneo yaliyoshuhudia mabadiliko makubwa.

Peterson Maelo sasa atakuwa kamanda mpya wa polisi kaunti ya Mombasa, huku Francis Wanjohi akisalia kamanda mkuu wa polisi ukanda wa pwani.

Manase Musyoka sasa ni kamanda mkuu wa polisi Kaunti ya Garissa.

Aliyekuwa mkuu wa polisi kaunti ya Mombasa Kipkemboi Rop sasa ni Kamanda wa polisi kaunti ya Taita Taveta.

Mkuu wa polisi eneo la Changamwe mjini Mombasa Joseph Muthee amehamishwa hadi ukanda wa bonge la ufa kama mkuu wa idara ya trafiki, nafsi yake ikichukuliwa na Stephene Chateka.

Aliyekuwa msemaji wa polisi Zipporah Mboroki sasa ni mkuu wa polisi wa eneo la llari.

Aliyekuwa OCPD wa Mombasa katika kituo cha Urban Geoffrey Mayek amehamishwa hadi jijini Nairob na sasa ni OCPD wa Buruburu.

Mji wa Kilifi na Malindi pia imepata manaibu wapya wa  polisi.

Mabadiliko haya yanatarajiwa kuimarisha usalama haswa katika maeneo yaliyoathirika na utovu wa usalama.

Comments

comments