Ramadhan Seif Kajembe ateuliwa mwenyekiti wa Kenya Ferry

Ramadhan Seif Kajembe ateuliwa mwenyekiti wa Kenya Ferry

by -
0 934
Ramadhan Kajembe ambaye ameteuliwa mwenyekiti wa Kenya Ferry. PICHA: HISANI

Nairobi, KENYA: Rais Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika usimamizi wa mashirika kadhaa humu nchini.

Mbunge wa zamani wa Changamwe Ramadhan Seif Kajembe ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa shirika la Kenya Ferry.

Rais pia amemteua aliyekuwa mkuu wa majeshi Julius Karangi kusimamia mamlaka ya viwanja vya ndege nchini na kumsimamisha kazi David Kimaiyo aliyemteua kusimamia mamlaka hiyo mwezi Disemba mwaka jana,

Ronald Osumba ambaye alikuwa mgombea mwenza wa mgombea urais mwaka wa 2013 Peter Keneth, ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Bodi ya hazina ya vijana.

Mbunge wa zamani wa Bumula Bifwoli Wakoli ameteuliwa  mwenyekiti wa shirika la maendeleo ya kilimo nchini naye Patrick Osero ameteuliwa mwenyekiti wa bodi ya shirika la hazina ya utalii.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES