Sherehe za kula nyama ya Mbwa zanoga nchini Uchina

Sherehe za kula nyama ya Mbwa zanoga nchini Uchina

by -
0 575
Wanunuaji wakichagua nyama ya Mbwa watakayonunua huko Yulin, Uchina.

Yulin, CHINA: Sherehe kubwa za kula nyama ya Mbwa zimeanza nchini Uchina licha ya pingamizi kutoka kwa watetezi wa haki za wanyama nchini humo.

Sherehe hizo zimenoga zaidi katika mji wa Yulin, ulio kusini mwa Uchina.

Wauzaji wanachinja mbwa na kupika nyama yao kisha kuisambaza kwa hoteli nyingi katika mji huo.

Takriban Mbwa elfu 10 wanatarajiwa kuchinjwa katika muda wa siku kumi hivi zijazo.

Watetezi wa  haki za wanyama wamekuwa wakiandamana kupinga sherehe hizo lakini juhudi zao hazikufua dafu.

Sherehe hizo ni za kila mwaka lakini watetezi hao wanataka zipigwe marufuku.

Wauzaji mbwa hata hivyo wanadaiwa kupata mbwa wengi kwa kuwaiba kutoka kwa watu mbalimbali huku mbwa wengine wakidaiwa kutolewa barabarani.

Yang Yuhua mtetezi wa haki huko Uchina, amenukuliwa va vyombo vya habari vya kimataifa akisema nao pia wamelazimika kununua Mbwa hao ili kujaribu kupunguza idadi ya mbwa watakaochinjwa mwaka huu.

“ tumekuja kuambia watu hapa kwamba Mbwa ni rafiki zetu. Hawafai kuwaua mbwa kwa njia hii ya kikatili.. tena la kusikitisha zaidi mbwa wengi wanaouawa ni wa kufugwa manyumbani.” Yuhua alisema.

Mbwa kati ya elfu 10 hadi elfu 20 huchinjwa kila mwaka katika sherehe hizi mjini Yulin, lakini pingamizi ya sherehe hizi zimeanza kushuhudiwa kutoka pande nyingi.

Imearifiwa kuwa Mbwa wanaochinjwa husafirishwa kwa karibu kilomita elfu 2 kutumia magari maalum bila kupewa chakula wala maji.

Lakini kuna wasiwasi wa kupata maradhi yanayohofiwa kusababishwa na nyama ya mbwa hasa kwa watu wanaokula nyama hiyo.

Miongoni mwa magonjwa yaliyo na urahisi wa kuambukiza watu hao ni kipindupindu na kichaa cha mbwa, maambukizi ambayo ni hatari sana.

Ripoti ya shirika moja la kibinadamu nchini humo inaonesha kuwa mji wa Guangxi ni kati ya miji mitano iliyo na idadi kubwa ya watu walioambukizwa kichaa cha mbwa huku mji wa Yulin, ukiwa mji ulio na visa vingi zaidi nchini humo.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES