Washukiwa wa al shabaab wakamatwa Kwale

Washukiwa wa al shabaab wakamatwa Kwale

by -
0 456

Kwale, KENYA: Polisi kaunti ya Kwale wamewakamata watu 5 wanaowahusisha na kundi la kigaidi la al shabaab.

Maafisa hao  wanasema wamewakamata katika msitu wa mbita eneo la kinango.

Hii inafikisha 9, idadi ya washukiwa wa kundi hilo ambao wamekamatwa katika muda wa siku mbili zilizopita.

Washukiwa hao wanaaminika kuhusika na mauaji tata ya wazee wa vijiji eneo hilo majuma mawili yaliyopita.

Mshukiwa mwingine aliuawa hapo jana kwa kupigwa risasi na kikosi maalum cha GSU.

Guruneti ,vyombo vya kupikia, pikipiki na visu vimepatikana ndani ya msitu huo.

Kamanda wa polisi eneo la pwani Francis Wanjohi amesema washukiwa wanazuiliwa kaika kituo cha polisi cha kinango kwa mahojiano  zaidi.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES