Wakaazi waliosalia karibu na msitu wa boni watakiwa kuondoka haraka

Wakaazi waliosalia karibu na msitu wa boni watakiwa kuondoka haraka

by -
0 392
Police officers patrolling Boni forest in Lamu. PHOTO:FILE

Mombasa, KENYA: Idara ya usalama pwani inawataka wakaazi wanaosalia karibu na msitu wa boni huko Lamu kuondoka maeneo hayo.

Mshirikishi mkuu wa usalama eneo la pwani Nelson Marwa anasema maeneo hayo bado ni hatari kufuatia oparesheni ya kiuslama inayoendeshwa na jeshi la KDF katika msitu huo.

Mwarwa anasema baadhi ya wakaazi wamekuwa wakijitengea  mashamba katika msitu huo.

Wakaazi wanaoagizwa kuondoka ni wale waliosalia baada ya wenzao kuhama sehemu hiyo wakati wa kuzindua oparesheni ya kiusalama ya “Linda boni” mwezi Septemba mwaka jana.

Marwa anasema kwa sasa usalama Lamu umeimarika na bado wanaendelea na mikakati ya kuwasaka magaidi wa alshabab wanaoendelea kutatiza usalama hapa nchini.

Amesema  wameboresha mikakati ya kukabiliana na magaidi hasa kufuatia shambulio la Jumatatu huko Mandera ambapo wanajeshi 5 waliuwawa na magaidi wa alshabab.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES