Raila akutana na Kuria pamoja na “Pangani 6” kwa chakula

Raila akutana na Kuria pamoja na “Pangani 6” kwa chakula

by -
0 444

Nairobi,KENYA:Kinara wa CORD Raila Odinga amekutana na mbunge wa Gatundu kusini Moses Kuria pamoja na viongozi waliokamatwa kwa tuhuma za uchochezi kabla ya kuachiliwa.

Walikutana kwa chakula cha mchana katika hoteli moja maarufu mjini Nairobi, siku chache baada ya wabunge hao kuachiliwa kutoka korokoroni.

Mkutano huo pia umewakutanisha kwa mara ya kwanza Raila na Kuria, tangu mbunge huyo adaiwe kutoa matamshi ya kutaka kinara huyo wa CORD auawe.

Lakini haikubainika ni kipi walichozungumzia wawili hao hasa baada ya matamshi tata ya Kuria kumhusu Raila.

Baadhi ya wabunge na maseneta hao waliokamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Pangani kwa siku nne ni pamoja na mbunge wa Suna mashariki Junet Mohammed, mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kilifi Aisha Jumwa,seneta wa Machakos Johnston Muthama.

Wengine ni mbunge wa Bahati kaunti ya Nakuru Kimaniu Ngunjiri na mbunge wa Kabete Ferdinand Waititu.

Mkutano huo pia umekuja siku kadhaa baada ya Raila kutangaza hadharani kwamba amemsamehe Kuria kwa tamko lake la kutaka auawe.

Raila alinukuliwa akisema Kuria hakumaanisha alichosema ila “alipagawishwa” na umati mkubwa wa watu.

Raila pia aliandamana na vinara wenza Moses Wetangula na Kalonzo Musyoka.

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Mombasa Mishi Mboko pia alihudhuria kikao hicho.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES