Maafisa watano wa polisi wauawa na Al-shabaab

Maafisa watano wa polisi wauawa na Al-shabaab

by -
0 282

Mandera,KENYA:Maafisa watano wa polisi wameuawa huko Mandera kwa kile kinachoaminika ni shambulio la wanamgambo wa al-shabaab wanaotoka nchini Somalia.

Walifariki wakati gari lao lilipolipuliwa walipokuwa wakisindikiza basi la abiria kulipatia ulinzi.

Gari la polisi hao lilishambuliwa kutumia roketi ya kurushwa kwa mkono eneo la Dabacity karibu na Elwak.

Gavana wa Mandera Ali Roba amelaumu polisi kwa kupuuza ripoti za kijasusi kuhusu uwezakano wa shambulio.

Haya yanajiri huku idara ya usalama ikitoa tahadhari kwa watu kuwa makini kufuatia vitisho vya kundi hilo la alshabaab.

Serikali ilisema Al-shabaab inataka kushambulia Kenya wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES