Mahakama yaruhusu uchunguzi wa sehemu za siri kwa wanaohusishwa na mapenzi ya...

Mahakama yaruhusu uchunguzi wa sehemu za siri kwa wanaohusishwa na mapenzi ya jinsia moja

by -
0 349

Mahakama kuu ya Mombasa imetupilia mbali ombi lililowasilishwa na wanaume wawili wanaodaiwa kuwa wapenzi, kupinga uchunguzi wowote wa sehemu za siri za wanaume kwa lengo la kubaini ikiwa huonana kimwili.

Wanaume hao waliwasilisha ombi hilo wakidai uchunguzi waliofanyiwa sehemu zao za siri ulikiuka katiba, na pia walitaka ushahidi kuhusu uchunguzi huo usitumike katika kesi inayowakabili, ambapo wanadaiwa kuwa wapenzi wa jinsia moja.

Akitoa uamuzi wake, Jaji Anyara Emukule amesema sheria inaruhusu wapenzi wa jinsia moja kufanyiwa uchunguzi wa sehemu za siri.

Emukule pia amesisitiza kuwa uchunguzi wa sehemu za siri za walalamishi ulifanywa kufuatia agizo la mahakama.

Awali Caleb Omar Idris na George Maina Njeri walishtakiwa kwa madai ya kuwa wapenzi wa jinsia moja kinyume na katiba.

Uamuzi huo umetolewa baada ya washukiwa kushtaki waziri wa kitaita wa afya, hakimu wa mahakama ya Ukunda, afisa wa upelelezi wa kituo cha polisi cha Msambweni, kiongozi wa mashtaka na hospitali ya Coast General, wakisema hawakutendewa haki wakati wa uchunguzi huo.

Pia walitaka wafidiwe wakidai waliumizwa wakati wa kufanyiwa uchunguzi huo wa sehemu zao za siri.

Uamuzi huo una maana kuwa wanaodaiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja sasa wanaweza kufanyiwa uchunguzi wa sehemu zao za siri ili kubaini ukweli.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES