Mwanamke “mchawi” ashambuliwa baada ya kufumaniwa na wakazi

Mwanamke “mchawi” ashambuliwa baada ya kufumaniwa na wakazi

by -
0 1413
Bidhaa za ushirikina PICHA:MTANDAO

Mombasa,KENYA:Mwanamke anayesemekana kuwa “mchawi’, ameshambuliwa na umati katika mtaa wa Soko Mjinga eneo la Kisauni hapa Mombasa.

Inadaiwa amekamatwa mapema leo alfajiri baada ya wenzake wawili kutoroka.

Kwa mujibu wa wakaazi, mwanamke huyo alikuwa “uchi wa mnyama” wakati alipofumaniwa juu ya paa la nyumba ambapo alishambuliwa.

Baadae wakazi waliokuwa na ghadhabu wamemwua kwa kumchoma moto wakitumia magurudumu ya gari.

Wakazi wanadai kuwa mwanamke huyo ni “mwanga’, ambaye amekua akiwahangaisha katika mtaa huo wa Soko Mjinga.

Duru zinasema kuwa alishambuliwa baada ya kushindwa kujieleza kuhusu ni nini alichokua akifanya juu ya paa la nyumba akiwa “uchi wa mnyama”.

Waliomshambulia wanasema mwanamke huyo licha ya kupewa kichapo cha mbwa hakuweza kuzungumza wala kuonyesha hisia zozote.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES