CORD yaahirisha maandamano yake huku ikiionya serikali

CORD yaahirisha maandamano yake huku ikiionya serikali

by -
0 302
NASA flag bearer Raila Odinga and his running mate Kalonzo Musyoka and co principal Moses Wetangula PHOTO COURTESY

Mombasa,KENYA:Muungano wa upinzani nchini CORD umetangaza kuahirihs maandamnao dhidi ya tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC yaliyofaa kurejelewa leo jumatatu.

Kinara wa CORD Raila Odinga, amesema wameahirisha maandamano hayo ili kuipa serikali hadi jumanne wiki hii kuafikiana nao kuhusu namna ya kuendesha mazungumzo ya kufanyia mageuzi IEBC.

Muungano huo unataka mazungumzo hayo yafanyike nje ya bunge badala ya kufanyiwa bungeni.

Tayari muungano huo na ule tawala wa Jubilee umewateua wanachama wa kamati itakayotwikwa jukumu la kuendesha mazungumzo hayo.

Lakini viongozi wa muungano huo wanasema watarejelea maandamano iwapo serikali itadinda matakwa yao.

CORD inataka makamishna wa tume hiyo ya uchaguzi waandamane.

Awali polisi ilikua imeiruhusu CORD kuandamana ila ikataka notisi ya njia ambazo waandamanaji watatumia na pia saa za mkutano kuisha.

Rais Uhuru Kenyatta alisema wana-CORD wana uhuru wa kuandamana mradi yawe ya amani.

Katika maandamano ya awali, ghasia zilishuhudiwa huku watu watatu wakiuawa.

Comments

comments