Usorovea wa mashamba kuanza mjini Voi

Usorovea wa mashamba kuanza mjini Voi

by -
0 422
Mbunge wa Voi Johnes Mlolwa. PICHA: HISANI

Voi, KENYA: Shughuli inatarajiwa kuanza hivi karibuni, kufanyia usorovea mashamba yaliyoko mjini Voi kaunti ya Taita Taveta, na kisha kutoa hati miliki za ardhi kwa wamiliki wa ardhi hizo.

Mbunge wa Voi Johnes Mlolwa anasema wizara ya kitaifa ya ardhi imeahidi kutuma masorovea kufanikisha shughuli hiyo.

Mlolwa anaamini ni hatua muhimu ya kumaliza mivutano ya mara kwa mara kuhusu mashamba miongoni mwa wenyeji wa Voi.

Idadi kubwa ya wa Voi wameishi katika ardhi zisizo na hati miliki kwa muda mrefu.

“Voi tuna shida ya titles. Watu wengi wako na letters of allotment lakini hawana title deeds. Watu wa wizara wamesema wananiletea surveyors tuzunguke Voi yote wananchi wapate title deeds zao. Nafikiri tukifika hapo serikali itakua imetusaidia, sasa wananchi wapate titles.” Alisema mbunge Mlolwa

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES