Ferry mbili zaidi kununuliwa Likoni hivi karibuni

Ferry mbili zaidi kununuliwa Likoni hivi karibuni

by -
0 310

Mombasa,KENYA:Serikali imetenga shilingi nusu bilioni za kununua feri mbili kutumika katika kivukio cha Likoni hapa Mombasa.

Akisoma makadirio ya bajeti ya taifa bungeni,waziri wa fedha Henry Rotich amesema hatua hiyo inalenga kupunguza msongamano wa watu na magari katika kivukio hicho.

Aidha serikali imeongeza shilingi bilioni 145 kwa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR.

Kuhusu elimu, serikali imetangaza kutenga shilingi bilioni 14 kwa uajiri wa walimu.

Rotich ametangaza kwamba mradi huo umekadiriwa kukamilika mwezi juni mwaka ujao.

Amedokeza kuwa tayari zabuni ya kukamilisha awamu ya pili ya mradi huo kuanzia Naivasha hadi mpakani mwa Kenya umekamilika.

Waziri huyo aidha ameongeza kuwa serikali imo mbioni kukamilisha miradi yote ya maendeleo iliyoanzisha.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES