Familia yaomba msaada kumsafirisha binti yao aliyekwama Uarabuni

Familia yaomba msaada kumsafirisha binti yao aliyekwama Uarabuni

by -
0 384

Kwale, KENYA: Familia moja Ukunda kaunti ya Kwale inaomba serikali na wahisani kuisaidia kumrejesha  nyumbami binti yao Aisha Ali Mwakufwairwa anayedaiwa kuzuiliwa nchini Saudia Arabia.

Kulingana na mamake mzazi Bi Mwanaida Juma, bintiye amelazimika kutafuta hifadhi katika kituo cha kuhifadhi wakimbizi nchini humo ili kukwepa kukamatwa baada ya kupokonywa vyeti vyake vya kusafiria na aliyekuwa mwaajiri wake.

Mwanaida anasema bintiye alisafirishwa kuelekea Uarabuni na maajenti mwaka 2014 kufanya kazi ya nyumbani lakini baadaye alitoroka kufuatia mateso aliyokuwa akipitia mikononi mwa mwajiri.

Afisa katika shirikia la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika Francis Auma ameambia Baraka FM kuwa juhudi zao za kumfikia wakala aliyemsafirisha msichana huyo hadi  Saudi Arabia hazijafaulu.

Lakini Auma amesema wanazungumza na idara za serikali ili kutafuta mbinu za kumsaidia msichana huyo.

Kabla ya kusafirishwa Uarabuni Aisha Ali Mwakufwairwa alikuwa mwanafunzi katika taasisi moja ya mafunzo mjini Mombasa.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES