Mahakama kuu yaunga mkono maandamano ya CORD dhidi ya IEBC

Mahakama kuu yaunga mkono maandamano ya CORD dhidi ya IEBC

by -
0 586
Wafuasi wa CORD wakiandamana Migori. PICHA: HISANI

Nairobi, KENYA: Mahakama kuu imepinga ombi la kutaka kuzuia maandamano ya wafuasi wa CORD dhidi ya tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.

Mahakama hiyo ya Nairobi badala yake, imesema ni sawa CORD kuendelea na maandamano hayo lakini yafanyike kwa amani.

Imemtaka inspekta generali wa polisi Joseph Boinnet kuhakikisha sheria na utulivu vinafuatwa wakati wa maandamano hayo.

Hayo yanajiri huku CORD ikikiuka agizo la polisi na kuendelea na maandamano Nairobi, na miji mingine nchini japo polisi wanajaribu kuzuia waandamanaji .

Huko Kibra Nairobi, baadhi ya biashara na hata shule zimeripotiwa kufungwa kwa kuhofia uharibifu.

Lakini idadi kubwa ya polisi wamekewa katikati mwa jiji hilo la Nairobi kuzia waandamanaji dhidi ya kuingia mjini baada ya idara ya usalama kusema maandamano hayo ni haramu.

Wafuasi wa CORD pia wanaandamana katika miji ya Migori na pia Busia

Katika mji wa Mombasa hali imekuwa shwari na hakujaonekana watu wanaokusanyika kwa maandamano hayo.

Vinara wa CORD wanasema hawana imani na maafisa wakuu wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC hivyo wanapaswa kuondoka mamlakani kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Juma lililopita wakati wa maadhimisho ya siku ya Madaraka, CORD iliipa serikali makataa ya siku mbili kuwasilisha orodha ya majina ya watu wataokutana na wenzao wa CORD kujadiliana kuhusu suala hilo la IEBC.

CORD imerejelea maandamano Jumatatu baada ya serikali kupuuza makataa hayo.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES