Afisa wa polisi apoteza bunduki yake kwa njia isiyoeleweka

Afisa wa polisi apoteza bunduki yake kwa njia isiyoeleweka

by -
0 266

Mombasa,KENYA:Watu wasiojulikana wamevamia kituo cha polisi cha likoni na kutoweka na bunduki.

Taarifa zinasema afisa mmoja wa polisi aliyekuwa zamu usiku alipoteza bunduki yake ya G3 kwa njia ya kutatanisha mapema jumamosi.

Inasemekana afisa huyo alikuwa ametoka chumbani kwake alfajiri lakini aliporejea akapata mlango wa nyumba yake imevunjwa na bunduki kuibwa.

Afisa huyo tayari ameandikisha taarifa na kitengo cha upelelezi huku juhudi za kutafuta bunduki hiyo zikianzishwa.

Mkuu wa polisi likoni Willy Simba amelidhibitisha taarifa hiyo.

Tukio hili linajiri miezi mitano baada ya afisa mwengine wa polisi kuuawa na watu wasiojulikana ambao baadaye waliiba bunduki yake.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES