Washukiwa wa MRC waachiliwa huru na mahakama

Washukiwa wa MRC waachiliwa huru na mahakama

by -
0 214

Mombasa,KENYA:Mahakama ya Mombasa imewaachilia huru washukiwa 43 wa kundi la Mombasa republican council-MRC.

Washukiwa hao Harun Nduria, Mambo Baya, Fredrick Kazungu pamoja na wengine 40 wameachiliwa baada ya kiongozi wa mashtaka kukosa kuwasilisha mashahidi mahakamani kwa muda wa miaka miwili.

Vijana hao walikamatwa mwezi disemba mwaka 2014 eneo la Kaloleni kaunti ya Kilifi.

Awali mahakama iliagizia washukiwa waachiliwe kwa dhamana ya shilingi laki tano kila mmoja au pesa taslimu shilingi elfu 80 baada ya kukana shtaka hilo.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES