NACADA yataka vilabu vya kuuza pombe vifungwe Mombasa

NACADA yataka vilabu vya kuuza pombe vifungwe Mombasa

by -
0 355

Mombasa:KENYA:Mshirikishi mkuu wa mamlaka ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya NACADA ukanda wa pwani sheikh Juma Ngao, anaitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kufunga vilabu vyote vya kuuza pombe, na ambavyo vinakiuka maadili.

Ngao alisema baadhi ya vilabu hivyo vilijengwa karibu na shule na maeneo ya kuabudu, na wanaoathirika zaidi ni watoto na vijana.

Akizungumza wakati wa sherehe za siku ya madaraka mjini Mombasa, Ngao aliongeza kuwa utafiti wa NACADA umeonyesha kuwa kati ya watoto 10 wenye umri wa miaka 12 na zaidi, wanne kati yao ni waraibu wa pombe na mihadarati.

Comments

comments