Viongozi wa CORD hatimaye wakutana na rais

Viongozi wa CORD hatimaye wakutana na rais

by -
0 378

Nairobi, KENYA: Viongozi wa mrengo wa CORD Raila Odinga na Moses Wetangula wamekutana na rais Uhuru Kenyatta kwa kile kinachoaminika ni kujadili kuhusu suala la tume ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Mkutano umekua ukiendelea Jumanne mchana katika ikulu ya rais Mjini Nairobi.

Hapo jana, wabunge wapatao 50 wa mrengo wa Jubilee na CORD walijadiliana mchana kutwa na kukubaliana kuhusu umuhimu wa kufanya mazungumzo ya kutafuta uvumbuzi kwa suala hilo la IEBC.

Mapema Jumanne, Raila Odinga alihudhuria ibaada ya maziko huko Narok lakini akaomba waombolezaji ruhusa ya kuondoka akisema alipokea simu kutoka kwa rais, aliyetaka wakutane katika ikulu saa nane mchana.

Alinukuliwa akisema atafahamisha wakenya kitakachojiri baada ya mazungumzo hayo.

Alienda kuhudhuria maziko ya mke wa aliyekuwa senata wa kwanza katika bunge la zamani, Bwana Lemein Kijiji cha Motonyi, kaunti ndogo ya Narok Kaskazini.

Awali muungano wa CORD ulipanga maandamano kwa muda wa majuma matatu mfululizo kutaka maafisa wakuu wa IEBC waondoke mamlakani lakini wakasitisha maandamano hayo kupisha mazungumzo.

 

Comments

comments