Wazee wawili na kiongozi wa dini wauawa kinyama

Wazee wawili na kiongozi wa dini wauawa kinyama

by -
0 356

Kwale,KENYA:Watu watatu wakiwepo wazee wawili wa vijiji na kiongozi mmoja wa kidini wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika katika kijiji cha Bongwe Ukunda kaunti ya Kwale.

Inasemekana genge la watu waliojihami kwa bunduki lilivamia kijiji hicho na kuwaamuru wakaazi kutotoka nje kabla ya kuwapiga risasi ya kichwa watu hao.

Duru za kijasusi zimeeleza kuwa washukiwa wa kundi la kigaidi eneo hilo wamekuwa wakilenga vijana walioasi kundi la Alshabab na kujisalimisha kwa serikali.

Kundi hilo pia limekua likiwalenga wazee wa vijiji na mabalozi wa nyumba kumi na hata viongozi wa serikali.

Kwingineko Polisi wa kitengo cha flying squad hapa Mombasa wanasema wamemkamata mshukiwa hatari wa mauaji katika kivuko cha ferry eneo la Likoni.

Polisi inasema imekuwa ikishirikiana na vitengo tofauti vya kiusalama kumsaka mshukiwa huyo aliyetambulika kwa jina Adam Mustafa Juma.

Mshukiwa anadaiwa kuongoza makundi hatari eneo la Majengo hapa Mombasa na anahusishwa pia na mauaji ya watu kadhaa.

Polisi pia inamhusisha mshukiwa huyo na kundi la kigaidi la al-shaab.

Mkuu wa polisi likoni Willy Simba aliiambia Baraka fm mshukiwa alikuwa anakwepa msako wa polisi huko Majengo na kujificha likoni.

Comments

comments