Wawakilishi wa wadi wataka uchaguzi mkuu uandaliwe 2018

Wawakilishi wa wadi wataka uchaguzi mkuu uandaliwe 2018

by -
0 276

Mombasa, KENYA: Muungano wa wawakilishi wa wadi nchini unasema hatua ya tume ya uchaguzi IEBC ya kuandaa uchaguzi mkuu mwaka 2017 itawanyima haki yao ya kuhudumu kwa miaka 5 kwa mujibu wa sheria.

Mwenyekiti wa muungano huo nchini Dr. Nur Nasir anasema muda wao wa kuhudumu unapaswa kukamilika mwezi Machi mwaka 2018 kulingana na katiba, na kuitaka tume ya uchaguzi kutathmini suala hilo.

Wawakilishi hao wametishia kuwasilisha kesi mahakamani iwapo pendekezo lao halitaangaziwa.

Wamekuwa katika kongamano la siku nne mjini Mombasa kuchanganua kuhusu maswala muhimu yanayofungamana na majukumu yao.

Comments

comments