Wafungwa wa nchi za nje kurejeshwa kwao

Wafungwa wa nchi za nje kurejeshwa kwao

by -
0 240

Mombasa, KENYA:Kuna uwezekano wafungwa wasio wakenya kwenye magereza ya humu nchini wakarudishwa makwao.

Hii ni kufuatia mazungumzo ya idara ya magereza hapa nchini na wawakilishi wa idara za magereza wa Rwanda na Uganda.

Micah Powon ambaye ni katibu mkuu wa idara ya magereza humu nchini, alisema wanaendelea kujadili swala hilo, na pia watafanya mazungumzo na mataifa mengine.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya jumatano, Powon alisema itakuwa bora wafungwa wa kigeni kutumikia vifungo nchini mwao ili kutatua changamoto za lugha na pia kuwa karibu na familia zao.

Comments

comments