Wakuu wa idara ya trafiki pwani wakaguliwa

Wakuu wa idara ya trafiki pwani wakaguliwa

by -
0 343
Mwenyekiti wa tume ya huduma kwa polisi Johnstone Kavuludi

Mombasa, KENYA: Maafisa wapatao 200 wa polisi wanaohudumu katika idara ya trafiki eneo la Pwani wameanza kukaguliwa mjini Mombasa.

Ukaguzi huo ulianza rasmi Jumanne.

Mwenyekiti wa tume ya huduma kwa polisi  Johnston Kavuludi anasema maafisa wanakaokaguliwa ni wa cheo cha Constable.

Kavuludi vilevile amesema zoezi hilo linalenga kubaini utendakazi na uadilifu wa maafisa wa trafiki.

Amedokeza kuwa maafisa wa polisi 33 tayari wameachisha kazi kote nchini  baada ya kukutwa na makosa mbalimbali yaliyobainika wakati wa ukaguzi ulioendeshwa awali.

Zoezi hilo litadumu kwa majuma mawili.

Comments

comments