Wafuasi wa CORD Mombasa waagizwa kuelekea ofisi za IEBC

Wafuasi wa CORD Mombasa waagizwa kuelekea ofisi za IEBC

by -
0 353

Viongozi wa CORD mjini Mombasa wameagiza wafuasi wa muungano huo kukwepa polisi wanaoshika doria na kuelekea hadi katika ofisi za IEBC hapa Mombasa.

Hii ni baada ya maafisa wa kulinda usalama Mombasa kutibua maandamano ya CORD yaliyonuiwa kuanzia katika bustani ya Uhuru hadi kwa ofisi za IEBC.

Maagizo hayo yametolewa na Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho aliyeandamaa na mbunge wa Mvita Abdulswammad Sharif Nassir katika bustani ya Uhuru mjini Mombasa.

Watu saba wamekamatwa katika eneo hilo walipojaribu kuongoza maandamano wakiwemo spika wa bunge la Mombasa Thadius Rajwai na wawakilishi kadhaa wa wadi.

 

Comments

comments