Spika wa Bunge la kaunti ya Kwale atangaza rasmi kuwania ugavana

Spika wa Bunge la kaunti ya Kwale atangaza rasmi kuwania ugavana

by -
0 483
Spika wa Kwale Sammy Ruwa. PICHA: HISANI

Kwale, KENYA: Spika wa bunge la kaunti ya Kwale Sammy Ruwa sasa ametangaza rasmi kuwania kiti cha ugavana wa Kwale  katika uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Ruwa ametangaza azma ya kumrithi gavana wa sasa Salim Mvurya kupitia tiketi ya chama cha ODM.

Ametangaza kutumia tiketi ya ODM licha ya fununu zilizoenea hapo awali kuwa angejiunga na mrengo wa Jubilee.

“Na nashukuru Mungu kwa kuwa hata gavana wetu wa sasa yuko ODM na mimi sitashtuka. Niko tayari kupambana na yeye kwa chama. Akinishinda kwa uwazi mimi sitakuwa na budi ila kumsupport. Nami nikimshinda na najua nitamshinda..pia yeye asianze mambo ya kukimbia kwa vyama vingine.. tubaki kwa ODM.” Alisema Ruwa alipohutubia mkutano wa CORD eneo la Lungalunga kaunti ya Kwale.

Awali, azimio la spika huyo  kutaka kuwania ugavana lilikosolewa na viongozi kadhaa wa serikali ya Kwale na hata wengine wa bunge la kaunti hiyo waliosema azma yake inaweza kutatiza utendakazi wake kama spika.

Amesema sera yake kuu ni kuinua kaunti ya Kwale kiuchumi na kwamba hawezi kubadili msimamo wake.

Comments

comments