Familia moja Likoni yashangazwa na habari za mwanao kuhusishwa na ugaidi

Familia moja Likoni yashangazwa na habari za mwanao kuhusishwa na ugaidi

by -
0 558

Mombasa,KENYA:Familia ya mshukiwa wa ugaidi aliyekamatwa mjini Moyale kaunti ya Wajir juma lililopita inasema imeshangazwa na taarifa za mwanao Juma Rashid Mwakimako, kukamatwa akidaiwa kuwa safarini kuelekea nchini Somalia.

Mamake mshukiwa Mwanamgeni Abdalla alisema alipata habari hizo kwenye vyombo vya habari kuwa mwanawe amekamatwa.

“Nilikuwa nimekaa mle ndani, akaja akaniambia mama nasafiri, naondoka, nikamwuliza waenda wapi? akanijibu wewe niombee”, amesema mamake mshukiwa.

Katika mahojiano ya pekee na Baraka fm nyumbani kwake eneo la Mrima-Likoni mjini Mombasa, Mwanamgeni alisema mwanae anawiki tatu tangu aondoke nyumbani.

Sasa anaiomba serikali imwachilie mwanawe akisema huenda alihadaiwa na mitandao ya watu wenye nia mbaya.

Babake mshukiwa alidai Ali Juma Mwakimako, alidai mwanawe amekuwa mtiifu na mwenye heshima kwa familia, japo hakuelewa jinsi mtoto wake alivyoondoka nyumbani.

Ali alisema amekuwa akipitia wakati mgumu baada ya kubaini mwanawe Rashid yuko mikononi mwa polisi wa kukabiliana na ugaidi.

Rashid alikamatwa pamoja na washukiwa wengine wanne huko Wajir wakielekea nchini Somalia, na wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga jijini Nairobi.

Comments

comments