Bunge la Mombasa laahirisha vikao huku CIPK ikilaani fujo za IEBC

Bunge la Mombasa laahirisha vikao huku CIPK ikilaani fujo za IEBC

by -
0 375
Ndani ya bunge la kaunti ya Mombasa.Vikao vimeahirishwa kufuatia fujo. PICHA:MAKTABA

Mombasa,KENYA:Bunge la kaunti ya Mombasa jumanne lilisitisha vikao vyake Kwa muda usiojulikana kufuatia tofauti zilizoshudiwa wiki iliyopita.

Wabunge wa kaunti ya Mombasa wanasema walichukua hatua hiyo ili kusuluhisha mzozo ulioko baina yao.

Wanasema wanatarajia kufanya mkutano na gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho kujaribu kutafuta suluhu.

Wabunge hao wa Mombasa wiki jana walizua vurugu na hata kupigana kutokana na shinikizo la baadhi yao kutaka kumuondoa spika wa bunge hilo Thadius Rajuay.

Kwingineko baraza la maimamu na wahuburi CIPK hapa Mombasa lilikashifu matukio ya jumatatu kwenye maandamano yalioongozwa na mrengo wa Cord kutaka makamishana wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC wang’atuke mamlakani.

Katibu wa baraza hilo Sheikh Mohammed Khalifa alisema yaliyojiri wakati wa maandamano mjini Nairobi, Kisumu na maeneo mengine, ni matukio ya kutia hofu kwa amani ya taifa na akasistiza wito wa majadiliano kati ya serikali na Cord.

Comments

comments