Mwanamume ajiua baada ya kupata mkewe ameolewa tena

Mwanamume ajiua baada ya kupata mkewe ameolewa tena

by -
0 304

Lamu,KENYA:Mwanamume mmoja amejiua kwa kujinyonga juu ya mti kwa madai mkewe amemtoroka na kuolewa kwingine.

Kisa hicho kimetokea eneo la Wiyoni kaunti ya Lamu.

Wakazi wanasema waliamka na kuupata mwili wa Jefwa Fisi, mwenye umri wa miaka 45 juu ya mti.

Kulingana na chifu wa Mkomani- Majid Basheikh,marehemu alikuwa ameenda bara Tana River lakini aliporudi akampata mkewe ameolewa.

Chifu huyo amedokeza kuwa huenda Fisi aligadhabishwa sana na usaliti wa mkewe ndiposa akaamua kujiua.

Mwili wa marehemu unahifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya Lamu.

Comments

comments