Basi la abiria nusura litumbukie baharini likoni feri

Basi la abiria nusura litumbukie baharini likoni feri

by -
0 613

Mombasa:KENYA:Msongamano mkubwa wa abiria pamoja na magari umeshuhudiwa katika kivuko cha feri eneo la likoni mjini Mombasa wakati basi moja la abiria lilipokaribia kutumbukia baharini.

Inasemekana basi hilo lililokuwa likitoka nchini Tanzania kuelekea mjini Mombasa, lilipoteza mwelekeo baada ya breki zake kufeli wakati likijaribu kuingia kwenye feri ili kuvukishwa hadi ng’ambo ya pili.

Basi hilo liliziba eneo moja la kuegesha feri na kusababisha msongamano mkubwa.

Hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa

Abiria wengi wamelazimika kusubiri huduma za feri kwa muda mrefu kutokana na tatizo hilo.

Comments

comments