Mombasa yaomboleza kifo cha mwanahabari wake

Mombasa yaomboleza kifo cha mwanahabari wake

by -
0 1299

Mombasa,KENYA:Fani ya uandishi wa habari hapa Mombasa inaomboleza kifo cha mwanahabari mwenzao.

Mwanahabari wa muda mrefu hapa Mombasa-Ngumbao Kithi, aliaga dunia jumatano katika hospitali ya Jocham akitibiwa.

Duru za habari zinasema kuwa Kithi amekua akiugua kwa muda mrefu.

Kulingana na mtu anayejiita rafiki yake kwenye ukurasa wa facebook, mwandishi huyo alisumbuliwa na maradhi ya moyo.

Kithi aliwahi kuwa mwandishi wa gazeti la The standard tawi la Mombasa ambapo amehudumu kwa muda mrefu.

Baraka FM inatuma risala za rambirambi kwa familia yake

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES