Polisi watibua mkutano wa “kidini” Mombasa

Polisi watibua mkutano wa “kidini” Mombasa

by -
0 476

Mombasa,KENYA:Polisi hapa Mombasa Jumatatu walitibua mkutano uliokuwa umeitishwa na kundi moja la viongozi wa kiislamu wa muungano wa Hizbul Tahir.

Duru zinaarifu kuwa mkutano huo uliitishwa kuhamasisha waislamu kuhusu utangamano baina ya dini mbalimbali.

Zaidi ya maafisa 50 wa polisi walifika katika ukumbi wa Islamic centre na kuamrisha watu wote waliokuwa ndani kuondoka.

Viongozi wa kiislamu kutoka Tanzania walikuwa baadhi ya wageni waliotarajiwa kuhutubia kongamano hilo.

Ustadh Shabaan Mwalimu ambaye ni mmoja viongozi walioalikwa kwenye kongamano hilo alikanusha madai kuwa mkutano huo ulikuwa na nia mbaya.

Kulingana na Shabaan, lengo lao ni kuleta uwiano na utangamano kati ya dini tofauti Mombasa.

Mkuu wa polisi hapa Mombasa Lucas Ogara aliambia Baraka fm mkutano huo haikuwa na kibali ila polisi walipata habari za kijasusi kuhusu mkutano.

“Tulipata habari hizi  na idara ya kijasusi,viongozi  walioandaa mkutano hawakuarifu polisi kulingana na sheria,tunafuatilia kwa karibu hata endapo watafanya mkutano  kama huo kwingine,”alisema Bw Ogara.

Comments

comments