Wazee wa mtaa Likoni wadai kuhangaishwa

Wazee wa mtaa Likoni wadai kuhangaishwa

by -
0 365

Mombasa, KENYA:Makundi ya vijana wanaotajwa kuwa hatari eneo la Likoni mjini Mombasa yanadaiwa kuanza kuwahangaisha wazee wa mtaa eneo hilo, wakiwataja kama wasaliti kwa vyombo vya usalama.

Baadhi yao wanadaiwa kutoroka makaazi yao wakihofia usalama wao.

Mzee wa mtaa wa Swabrina eneo hilo anadai kundi la vijana 5 waliokuwa wamejihami kwa panga na visu walifika nyumbani kwake, wakitaka kumshambulia usiku wa kuamikia alhamisi.

Anasema genge hilo limekuwa likifika nyumbani kwake kumsaka kwa lengo la kulipiza kisasi.

Mkuu wa polisi likoni Willy Simba anasema polisi watafanya kila wawezalo kuwanasa washukiwa hao.

Wakati huo huo idara ya usalama mjini Mombasa inapanga mikakati ya kutuma maafisa wa kupambana na ghasia GSU katika eneo hilo la Likoni kukabili makundi hayo vijana.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES