Mwili wa msichana wapatikana Likoni

Mwili wa msichana wapatikana Likoni

by -
0 417

Mombasa, KENYA:Mwili wa msichana aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule moja ya upili wilayani Likoni mjini Mombasa umepatika eneo la Shelly beach.

Wakaazi waliozungumza na Baraka Fm wamesema mwili huo ulikuwa ndani ya gunia na huenda msichana huyo alibakwa kabla ya kuuawa.

Mkuu wa polisi eneo hilo Willy Simba anasema babake msichana huyo Ezekiel Ambase alikuwa amepiga ripoti polisi kuhusu mwanawe kutoweka.

Inasemekana msichana huyo alitoweka nyumbani kwao wiki tatu zilizopita.

Mwili wa msichana huo unaifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya coast general mjini mombasa huku uchunguzi ukiendelea.

Comments

comments