Kesi “tata” yakosa kuendelea mahakamani Mombasa

Kesi “tata” yakosa kuendelea mahakamani Mombasa

by -
0 384

Mombasa,KENYA:Hakimu aliyekuwa akisikiza kesi mahakamani Mombasa kati ya familia zinazozozania kuuzika mwili wa msichana wao, amejiondoa na kutaka hiyo izikizwe na hakimu mwingine.

Hakimu Simon Rotich amesema anatilia shaka namna kesi hiyo ilivyokuwa ikiendeshwa.

Kesi hiyo ilikosa kusikizwa alhamisi hii baada ya mahakimu kutofautiana kuhusu nani wa kusikiza kesi hiyo.

Familia ya Isaac Njoroge na Zainabu Isaac zimekuwa zikizozania kuzika mwili wa msichana wao Yasmini Njoroge mwenye umri wa miaka 22 aliyefariki tarehe 11 mwezi machi mwaka huu.

Familia hizo zinataka kuuzika mwili wa binti huyo kulingana na dini zao tofauti.

Hakimu Douglas Ogoti ameagiza kesi hiyo kutajwa siku ya jumanne juma lijalo ili kutoa mwelekeo wa kesi hiyo kusikizwa.

Comments

comments