Waandishi wa Baraka FM washinda tuzo

Waandishi wa Baraka FM washinda tuzo

by -
0 497
Baraka FM's reporter Brian Osweta, holding his trophy after Media gala in Nairobi on Wednesday. PHOTO:COURTESY

Nairobi,KENYA:Baraka FM kwa mara nyingine imetambuliwa kwa kukuza vipaji.

Hii ni baada ya waandishi wake wawili kushinda tuzo za uandishi bora mjini Nairobi jumanne usiku.

Joseph Jira na Brian Osweta walishinda kupitia makala waliyoandika.

Jira alishinda katika kitengo cha biashara huku Osweta akishinda kupitia makala ya afya.

Huu ni mwaka wa tatu mfululizo kwa Baraka FM kushinda tuzo katika kitengo cha afya katika mashindano hayo ambayo huandaliwa kila mwaka.

Mashindano hayo yaliandaliwa na baraza la vyombo vya habari nchini (MCK).

Wanahabari wengine Oscar Nyoha,Diana Wanyonyi na Albert Mwangeka waliibuka wa pili katika vitengo vyao.

Mashindano hayo yalifanyika huku dunia ikiadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari.

Hapa Baraka FM tunasema hongera kwao

Comments

comments