Wanahabari wa Baraka FM wateuliwa tena kuwania tuzo za uandishi bora

Wanahabari wa Baraka FM wateuliwa tena kuwania tuzo za uandishi bora

by -
0 534

Mombasa,KENYA:Stesheni ya Baraka FM inayotamba kote mkoani Pwani kwa mara nyingine imejizoela sifa tele.

Wanahabari wake watano wameteuliwa kuwania tuzo za uandishi bora mwaka huu.

Tuzo hizo huandaliwa kila mwaka na baraza la vyombo vya habari nchini MCK.

Wanahabari hao ni pamoja na; Brian Osweta, Oscar Nyoha, Joseph Jira na Diana Wanyonyi pamoja na Albert Mwangeka.

Wameteuliwa kutokana na makala waliyoandika na kupeperushwa na Baraka FM.

Washindi watabainika kesho ambapo ni siku ya kuadhimisha uhuru wa vyombo vya habari,huku rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kuhudhuria tamasha hilo.

Mwaka jana Baraka FM pia ilitia fora baada ya wanahabari wake kutuzwa katika mashindano hayo mjini Nairobi.

George Otieno pamoja na Janet Kilalo walishinda tuzo katika kitengo cha afya,Joseph Jira akishinda kitengo cha teknolojia.

Mtangazaji gwiji-Josephat Kioko alishinda tuzo ya utawala bora,huku Oscar Nyoha na Diana Wanyonyi pamoja na Albert Mwangeka wakiibuka wa pili katika makundi yao.

Zawadi zilizotolewa zilikuwa pamoja na vikombe,vyeti na shilingi elfu 40 kwa kila mshindi wa kitengo.

Comments

comments