Miaka 22 tangu mkasa wa Mtongwe Ferry

Miaka 22 tangu mkasa wa Mtongwe Ferry

by -
0 575
Abiria wakisubiri kwa hamu kuvukishwa na ferry upande wa pili

Imetimia miaka 22 tangu kutokea mkasa wa  Mtongwe ferry ambapo Ferri ilizama na  zaidi watu 272 kufariki.

Mkasa huo wa Ferry ulitokea tarehe 29 Aprili mwaka 1994.

Mkasa huo unatajwa kuwa m-baya zaidi kuwahi kutokea katika kivukio cha kuvukisha abiria kutumia ferr .

Ferry kwa jina MV Mtongwe ilizama ilipokuwa ikivikusha abiria  kuelekea upande wa kisiwani kupitia maji ya bahari ya eneo la Kilindini.

Chombo hicho kilisemekana kuzama kwa kubeba abiria kupita kiasi.

Inaaminika zaidi ya watu 400 waliameabiri ferry hiyo badala ya idadi ya kawaida iliyopaswa kuwa abiria 300.

Baadhi ya wakaazi wa Mombasa wameambia Baraka fm bado wana kumbukumbu za siku hiyo.

Wanasema ilikuwa funzo kubwa na mikakati inapaswa kuwekwa na idara husika kuepuka mkasa mwingine kama huo.

 

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES