Marubani wa Kenya Airways wasitisha mgomo

Marubani wa Kenya Airways wasitisha mgomo

by -
0 355
Ndege ya shirika la Kenya Airways

Shirika la ndege nchini Kenya Airways limeanzisha tena safari zake za ndege baada ya marubani kusitisha mgomo wao.

Marubani walishiriki mgomo kukosoa baadhi ya hatua za usimamizi wa shirika hilo na kulazimu Kenya Airways kusitisha safari zote za ndege kuanzia Alhamisi jioni.

Usimamizi wa shirika hilo unasema kufikia Ijumaa saa sita mchana, ndege 22 zilikuwa zimekwishapaa angani kwa safari za humu nchini na pia za mataifa ya nje.

Muungano wa marubani kupitia katibu wao Paul Gichinga amedokeza kuwa usimamizi wa Kenya Airways umekubali baadhi ya mapendekezo waliyokuwa wakishinikiza lakini mazungumzo yataendelea hadi tarehe 1 mwezi Juni.

Muungano huo unakosoa baadhi ya hatua anazochukua mkurugenzi wa Kenya Airways Mbuvi Ngunze kujaribu kunusuru kampuni hiyo ambayo ilipata hasara katika mwaka wake wa kifedha uliopita.

Awali walitishia kugoma hadi Ngunze atakapojiuzulu wadhifa wa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo.

Kenya Airways ni miongoni mwa mashirika makubwa ya ndege barani Afrika na husafirisha angalau abiria elfu 10 kila siku

Comments

comments