Waziri wa ardhi kaunti ya Lamu mashakani

Waziri wa ardhi kaunti ya Lamu mashakani

by -
0 349

Lamu, KENYA: Bunge la kaunti ya Lamu Alhamisi hii linajadili ripoti ya kutokua na imani na  waziri wa ardhi Kaunti hiyo, Bi Amina Rashid.

Mjadala huo unakuja baada ya kamati maalum iliyoteuliwa kuchunguza mienendo ya waziri huyo  kuwasilisha ripoti mapema juma hili.

Kamati hiyo iliteuliwa baada ya bunge la Lamu kupitisha hoja ya kumtaka Bi Rashid ang’atuke ofisini likimhusisha na tuhuma za kuzembea kazini na pia ufisadi.

Upande wake Gavana wa Lamu Issa Timamy, anasema hatua ya kutaka kumuondoa waziri huyo mamlakani inachochewa kisiasa.

 

Comments

comments