Wakulima Mpeketoni hatimaye waridhia mradi wa kuzalisha nguvu za umeme

Wakulima Mpeketoni hatimaye waridhia mradi wa kuzalisha nguvu za umeme

by -
0 255

Lamu, KENYA: Wakulima huko Mpeketoni kaunti ya Lamu sasa wanasema wameridhia  mradi wa kuzalisha nishati utakaoanzishwa eneo hilo tofauti na kauli yao ya awali ambapo walisisitiza kupinga mradi huo.

Wakulima hao wamebadili nia baada ya kufanya mkutano na wawekezaji wa mradi huo na kuelezewa manufaa yake.

Hapo nyuma walitofautiana na wawekezaji kuhusiana na ardhi iliyotengewa mradi huo.

Mradi huo utakaogharimu Shilingi 21 bilioni unafadhiliwa na kampuni ya Electrawinds kutoka Ubelgiji, benki ya dunia, pamoja na Kampuni ya Kenwind Holdings ya humu nchini.

Mradi huo umetengewa jumla ya ekari 3,200 za ardhi katika eneo la  Baharini.

Unatarajiwa kuzalisha takriban megawati 90 za nguvu za umeme.

 

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES