Kesi inayomkabili mwanaharakati Mgandi Kalinga kuanza kusikilizwa

Kesi inayomkabili mwanaharakati Mgandi Kalinga kuanza kusikilizwa

by -
0 356
Mwanaharakati Mgandi Kalinga anayedaiwa kumtusi seneta mteule kupitia ujumbe mfupi

Mahakama ya Mombasa Alhamisi hii, itaanza kusikiliza Kesi ya utumiaji mbaya wa kifaa cha mawasiliano inayomkabili mwanaharakati wa Mombasa  Mgandi Kalinga.

Kalinga anadaiwa  kutuma ujumbe wa matusi kwa Seneta mteule  Emma Mbura kutumia mtandao wa kijamii wa whatsapp.

Awali, mshukiwa alikana shtaka hilo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili.

Vile vile alieleza mahakama kuwa aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mlalamishi Emma Mbura kwa muda mrefu, na kwamba uhusiano huo ulisambaratisha ndoa yake.

hapo nyuma, wakili wa mshtakiwa alitaka  mlalamishi amsamehe mteja wake kwa kuwa ni kiongozi na anafaa kuwa mfano mwema kwa raia.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES