Mvua kubwa na upepo mkali vyatabiriwa pwani na bonde la ufa

Mvua kubwa na upepo mkali vyatabiriwa pwani na bonde la ufa

by -
0 372

Nairobi, KENYA: Idara ya utabiri wa hali ya anga inatabiri mvua kubwa kuanzia Jumatano hadi Alhamisi katika sehemu nyingi za pwani ya Kenya na pia maeneo ya Bonde la ufa.

Idara hiyo inasema mvua hiyo inatabiriwa kufikia hadi kiasi ya milimita 40 siku ya Jumatano, na kuongezeka hadi milimita 50 Alhamisi.

Inatabiriwa kunyesha kwa  muda wa saa 24 na kuandamana na ngurumo za radi.

Sehemu zinazotarajiwa kuathirika zaidi ni za kusini mwa pwani kama vile Msambweni, Wasini Island na Shimoni, mjini Mombasa, Kilifi, Tana River na pia Lamu.

Maeneo mengine ni Kericho, Narok, Kisii na Bomet.

Wakaazi wa sehemu hizo wanahimizwa kuwa makini ili kuepuka athari zinazoweza kutokana na mvua hiyo.

Idara ya utabiri wa hali ya anga vile vile inahimiza wakaazi wa sehemu zinazotarajiwa kuathirika kufuatilia kwa vyombo vya habari, idara ya kukabiliana na majanga, Shirika la Red Cross, na mashirika mengine ya kukabiliana na matukio ya dharura, ili kufahamishwa zaidi kuhusiana na mvua hiyo inayotabiriwa.

 

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES