Wakaazi Tana River watofautiana na usimamizi wa fedha za bursary

Wakaazi Tana River watofautiana na usimamizi wa fedha za bursary

by -
0 283

Wakaazi wa kaunti ya Tana River wanasema hawaridhishwi na ugavi wa fedha za hazina ya karo yaani Bursary.

Mohamed Gedi mkaazi wa Tana River ameambia Baraka Fm kwamba wadi zote hutengewa kiwango sawa cha fedha hiyo licha ya tofauti ya idadi ya wanafunzi.

Gedi anasema kuna wadi zingine zilizo na wanafunzi zaidi ya elfu moja na zingine zilizo na hata wanafunzi 600 pekee ilhali wadi zote zinapewa mgao sawa wa fedha hiyo.

Lakini mwenyekiti wa bodi ya hazina hiyo Tana River  Abdi Hussein anasema ugavi wa fedha hiyo unatekelezwa kuambatana na sheria iliyopitishwa na bunge la kaunti.

Hussein amesisitiza kuwa hawawezi kubadilisha sheria hiyo hadi itakapofanyiwa marekebisho bungeni.

 

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES