Ujenzi wa ukuta mpakani mwa Kenya-Somalia kuendelea

Ujenzi wa ukuta mpakani mwa Kenya-Somalia kuendelea

by -
0 565
Ukuta unaojengwa kati ya Kenya na Somalia huko Lamu PICHA:MAKTABA

Lamu,KENYA:Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaisery anasema ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa Kenya na Somalia utaendelea.

Ukuta huo unaokadiriwa kuwa na upana wa Kilomita 700 unanuiwa kuzuia watu wanaoingia na kutoka humu nchini bila idhini.

Ukuta huo pia unalenga kuwazuia wanamgambo wa kigaidi wa Al-shabaab kuingia humu nchini kutekeleza mashambulizi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kiusalama jijini Nairobi siku ya Jumapili, Nkaisery alitoa wito kwa jamii zinazoishi mpakani kushirikiana na serikali ili kuhakikisha kuwa usalama unaimarishwa.

 

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES