Ashtakiwa kwa madai ya ulanguzi wa binadamu

Ashtakiwa kwa madai ya ulanguzi wa binadamu

by -
0 264

Mombasa, KENYA: Mwanamume ameshtakiwa mahakamani Mombasa kwa madai ya ulanguzi wa binadamu.

Mahakama imeelezwa kuwa Robert Msando Meti alikamatwa Alhamisi katika kivukio cha Likoni Ferry Mombasa, akisafirisha raia sita wa Ethiopia.

Mshukiwa amekana mashtaka mbele ya hakimu  Diana Mochache.

Raia wa Ethiopia wanaodaiwa kulanguliwa hawakusomewa mashtaka kwa sababu hakukuwa na mkalimani wa kusaidia katika mawasiliano.

Wataendelea kuzuiliwa  hadi Jumatatu watakaposhtakiwa kabla ya kesi kusikilizwa tarehe 16 mwezi Juni.

Walikamatwa katika kivukio cha Likoni Ferry wakitumia gari dogo aina ya Toyota Rav 4.

Polisi walitoa majina ya raia haow a Ethiopia kama Makengo Mamush Bekele, Madebo Dejene Ashore, Ashore Deslegn Detebo, Girma GabreLengu, Teketer Habichu Abaya, na Robert Msando Meti aliyeshtakiwa Ijumaa ambaye alikuwa dereva wa gari walilokuwa wakisafiria.

Yamkini walihojiwa na kusema walikuwa safarini kuelekea Lungalunga, kusini mwa pwani.

Comments

comments