Waathiriwa wa mafuriko huko Lungalunga wapata msaada

Waathiriwa wa mafuriko huko Lungalunga wapata msaada

by -
0 413
Wakaazi wa Tsuini Lungalunga kaunti ya Kwale waking'ang'ana kuvuka maji yaliyofurika kutokana na mvua kubwa. PICHA: HISANI

Zaidi ya familia 70 zilizoathiriwa na mafuriko huko Kiwegu Lungalunga kaunti ya Kwale zimepokea msaada kutoka kwa shirika la msalaba mwekundu, serikali kuu na pia serikali ya kaunti ya Kwale.

Msaada huo ni pamoja na chakula, neti za kukinga mbu, na maji safi.

Pia kumetolewa msaada wa kliniki tamba ili kufikia waathiriwa wanaohitaji matibabu katika sehemu mbalimbali eneo hilo .

Mkuu wa shirika la Redcross Abass Gullet anasema ni zaidi ya nyumba elfu 3 pamoja na wakaazi elfu 18 walioathirika.

Athari hizo zimetokana na mvua kubwa iliyonyesha kusini mwa pwani siku chache zilizopita.

Shughuli za usafiri zilitatizika kwa muda wa siku nne hivi eneo la Vanga huko Lungalunga baada ya mto umba kuvunja kingo zake na kusababisha mafuriko.

Mimea shambani pia imesombwa na maji.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES