Raia wa kigeni wakamatwa Likoni Ferry

Raia wa kigeni wakamatwa Likoni Ferry

by -
0 334

Mombasa, KENYA: Polisi mjini Mombasa wamewakamata raia 7 wa kigeni wanaohusishwa na kuwa humu nchini kinyume cha sheria.

Polisi wanasema watu hao saba ni raia wa Ethiopia.

Wamekamatwa wakiwa katika kivukio cha Likoni Ferry wakitumia gari dogo aina ya Toyota Rav 4.

Polisi wametoa majina yao kama Makengo Mamush Bekele, Madebo Dejene Ashore, Ashore Deslegn Detebo, Girma GabreLengu, Teketer Habichu Abaya, na dereva wa gari hilo Robert Msando Meti.

Yamkini wamehojiwa na kusema walikuwa safarini kuelekea Lungalunga, kusini mwa pwani.

Wanatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Ijumaa.

Comments

comments