Washukiwa 18 wa ujambazi wakamatwa na polisi

Washukiwa 18 wa ujambazi wakamatwa na polisi

by -
0 387
Administration Police in patrol. PHOTO/FILE.

Mombasa,KENYA:Polisi huko Changamwe wamewakamata watu  18 wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa makundi ya uhalifu “wakali wao” na “wakali kwanza” ambayo kwa muda sasa yametajwa kutatiza usalama hapa Mombasa .

Washukiwa hao walikamatwa katika maeneo ya Kalahari, Dunga unuse na Chaani.

Polisi wanasema “wahalifu hao” waliwakamata  na misokoto kadhaa ya bangi, pombe ya chang’aa na silaha .

Polisi pia wanasema wamegundua  kundi jipya lililochipuka linalojiita “The Spanish” ambalo wafuasi wake kadhaa ni miongoni mwa waliowakamata.

Hayo yanakuja siku moja tu baada ya wafuasi wengine 18 wa kundi la wakali wao  kukamatwa mtaa wa Majengo hapa Mombasa

Comments

comments