Mzee auwawa kwa kupigwa risasi Kwale

Mzee auwawa kwa kupigwa risasi Kwale

by -
0 399

Kwale,KENYA: Idara ya polisi eneo la mbuwani Ukunda huko wadi ya Bongwe gombato kaunti ya kwale jumatatu ilisema kuwa imeanzisha uchunguzi wa kisa cha mzee mmoja kupigwa risasi na kuuwawa na watu wasiojulikana.

OCPD wa msambweni Joseph Omija anasema kisa hicho kilitokea jumapili ambapo mzee kwa jina Boko Mohammed Mwakandandi alipigwa risasi nje ya nyumba yake majira ya jioni na watu wasiojulikana.

“Alikuwa ameketi akishughulikia na mabo ya jioni wakati watu wawili walkiuja na piki wakiwa armed na Ak 47 na bila kusema chochote wakampiga risasi na kutoweka bila kuiba chochote.” Alisema Omija.

Visa vya watu kuuwawa kwa kupigwa risasi na washukiwa kutoroka kwa pikipiki eneo la Ukunda vimeripotiwa kuzidi mwaka huu.

Comments

comments