Washukiwa wa genge la “kapenguria six” wakamatwa Likoni

Washukiwa wa genge la “kapenguria six” wakamatwa Likoni

by -
0 356

Likoni, KENYA: Polisi wilayani Likoni wanasema wamekamata genge la washukiwa wa uhalifu wanalosema ni la the “kapenguria six” linalohusishwa na kuhangaisha watu na pia uporaji wa mali eneo hilo.

Kulingana na polisi, washukiwa hao wamekamatwa katika ufukwe wa bahari wa Shelly beach baada ya kushambulia watalii, kuwapora mali na pia kuwajeruhi kutumia visu.

Mkuu wa polisi Likoni Willy Simba ametoa majina ya washukiwa hao kama Steve Owiti, David Murage, Mwalimu Suleiman na Brian Murage.

Simba amesema wamewanasa na mikufu ya dhahabu, kadi ya atm, na simu ya mkono.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES